Issue ya mzozo wa kidiplomasia inayoendelea kati ya nachi ya Korea Kaskazini na Marekani ni moja ya story ambayo inaendelea kumake headlines katika mitandao mbalimbali duniani kwa kipindi kirefu sasa na hauoneshi kupoa.
Pamoja na hayo nimekukusanyia story kubwa 7 ambazo zimepewa uzito wa juu kwenye twitter ikiwepo issue ya China kutoa msaada wa mchele kwa Kenya na mzozo wa kisiasa walioikumba Ufaransa.
Hizi ni Tweets 7 za story kubwa mchana wa leo June 22, 2017.
Serikali ya Korea Kaskazini imesema Rais Donald Trump ni mtu mwenye matatizo ya akili kwa kuingilia mambo yao wakati nchi yake haimwelewi. pic.twitter.com/LO7aQmwPAd
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017
Wafanyabiashara wa Mirungi kutoka Nyambene, Meru nchini Kenya wameiomba serikali iwaruhusu kusafirisha Mirungi kwenda Somalia kwa ndege #CRI pic.twitter.com/6Jg0X2ojrO
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017
Benki ya Maendeleo Afrika AfDB imezindua mkakati unaolenga kufungua nafasi milioni 25 za ajira kwa vijana wa Afrika ndani ya miaka 10 ijayo. pic.twitter.com/VshIt5qben
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017
Mgombea Urais kupitia upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema watafungua kesi kuzuia zabuni ya kampuni ya kuchapisha karatasi za kura. pic.twitter.com/CSbkflcurX
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017
Baada ya Mawaziri wa Ulinzi, Sheria na Mambo ya Ulaya wa Ufaransa kujiuzulu, Rais Macron amewateua watakaoshika nafasi zao jana hiyo hiyo. pic.twitter.com/kWLbelwwgG
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017
China imeipa Kenya mifuko 100,000 ya mchele kwa ajili ya walioathiriwa na ukame ni sehemu ya mifuko 450,000 iliyoahidiwa na serikali yake. pic.twitter.com/2IhiS1SZ1Z
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017
Malkia Elizabeth II wa Uingereza ametangaza kudumisha utulivu wa taifa na kuhakikisha nchi yake inajitoa kwenye Umoja wa Ulaya kwa utaratibu pic.twitter.com/19BxMD5cCQ
— millardayo (@millardayo) June 22, 2017