AyoTV

Mbowe na Matiko walivyorudishwa Mahakamani baada ya Mwaka Mpya (+video)

on

Leo January 3, 2019 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wamerudishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi yao ya uchochezi baada ya kusheherekea Krismasi na Mwaka Mpya wakiwa gerezani.

Mbowe na Matiko wanasota mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana yao November 26,2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana, ambapo waliamua kukata rufaa Mahakama Kuu lakini iliwekewa pingamizi baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa Mahakama ya Rufani.

Ayo Tv na Millardayo.com inayo full video jinsi Mbowe na Matiko walivyofikishwa mahakamani, ambapo pia wameweza kukutana na washtakiwa wenzao saba ambao ni viongozi wa CHADEMA.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16, 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

RUFAA YA MBOWE NA MATIKO: Mahakama yatoa majibu baada ya Profesa Safari kuhoji

Soma na hizi

Tupia Comments