AyoTV

Hali ya Ester Bulaya akiwa Hospital baada ya kuugua akiwa rumande

on

Usiku wa August 20 kulikuwa na taarifa kuhusu kuugua kwa Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya wakati akiwa rumande baada ya kukamatwa na Polisi Tarime ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya Tarime.

Ayo TV na millardayo.com zinaye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Hippolite Tarimo ambaye amesema hali ya Mbunge huyo inaendelea vizuri na tayari ameandikiwa rufaa ya kwenda Hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi.

Ester Bulaya aliugua akiwa rumande baada ya kushikiliwa na Polisi kufuatia kumkamata akiwa Hotelini Tarime August 19, 2017.

CHADEMA imethibitisha Ester Bulaya kukamatwa na Polisi…play hapa chini!!!

Soma na hizi

Tupia Comments