Habari za Mastaa

Swali analojiuliza G Nako kuhusu Ruge, hapati jibu

By

on

Kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG) Ruge Mutahaba kinaendelea kuwaumiza wasanii wengi, pamoja na kuwa Ruge amewagusa watu mbalimbali katika jamii kutokana na mambo ya kukumbukwa aliyofanya, mkali wa Weusi G Nako bado hataki kuamini.

Ruge ukiachana na kuwa kiongozi wa chombo cha habari lakini alikuwa ni mbunifu katika masuala ya sanaa, hivyo mkali wa Weusi G Nako, ameonesha kutambua mchango wa Ruge katika sanaa yake na kujiuliza bila Ruge itakuwaje? Ruge alikuwa kiini kikuu cha kuandaa matamasha kwa ustadi wa hali ya juu kama FIESTA na mengineyo.

G Nako ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa instagram  “💔💔💔ITAKUAJE BILA MWAMBA NAJIULIZA SIPATI JIBU!!! #RUGE Ruge alifariki February 2019 akiwa anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini, baada ya kuugua tatizo la figo kwa zaidi ya miezi minne.

VIDEO: ‘Ruge aliwahi kuniambia anafurahishwa na mahusiano yangu na Tunda’

Soma na hizi

Tupia Comments