Habari za Mastaa

Hela sio kitu kwa Davido, achagua kulitumikia jeshi la Nigeria

on

Superstar Davido ameamua kuahirisha show ya ziara yake ya ‘Davido Locked Up’ iliyotakiwa kufanyika Houston Dallas Marekani kutokana na muingiliano wa ratiba yake na kuamua kulitumikia jeshi la Nigeria ‘NYSC’ ikiwa amejiunga na mafunzo hayo kwa wiki tatu.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Davido ametoa taarifa hiyo ikiwa pia amesema yeye pamoja na management yake wanampango wa kurudisha pesa kwa wale ambao tayari walikuwa wamenunua tiketi na kusema kuwa tarehe rasmi zitapangwa kwa ajili ya show husika zilizoahirishwa.

“Kutokana na ratiba iliyoingiliana na jeshi la Nigeria NYSC tarehe zilizobakia kwaajili ya ziara ya ‘Davido Locked Up’ zimeahirishwa. Kiasi kitakachofidiwa ni cha gharama halisi ya ununuzi wa tiketi, Davido na timu yake watafanya kazi kwa bidii na kupanga tarehe mpya”

“Nawapenda sana na tutaonana Houston Dallas, LA na San Francisco nitawapa tarehe hivi karibuni,OBO”

Alikiba kamwambia Ommy Dimpoz “usiwaze Mungu kakunusuru wote si wake”

Soma na hizi

Tupia Comments