AyoTV

Ubalozi wa India ulivyoguswa na Elimu ya Tanzania

on

Ubalozi wa India nchini Tanzania leo August 10, 2017 umetoa msaada wa vitabu 1,030,000 vya masomo ya Hesabu, Fizikia, Baiolojia na Kemia kwa ajili ya Kidato cha Tatu hadi Kidato cha Sita kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa elimu nchini.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati akipokea msaada huo amesema kuwa vitabu hivyo vitagawanywa kwa kuzingatia shule zenye uhaba mkubwa wa vitabu nchini ili kuchochea ari ya kujifunza masomo ya sayansi.

Aidha, Waziri Ndalichako amesema Serikali ya India hivi karibuni imetoa msaada wa vifaa na wataalamu wa kufunga mitambo kwenye Chuo kipya cha kufundishia masomo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambacho kitatoa mafunzo kwa ngazi ya Masters kwa masomo hayo ikiwa ni pamoja na kupeleka Watanzania kusoma utaalamu huo nchini India.

Balozi wa India nchini Sandip Arya amesema anaamini vitabu hivyo vitaongeza thamani na motisha kwa wanafunzi wa Tanzania kusoma masomo ya sayansi.

Ulipitwa na hii? Kama unataka kuomba mkopo, kuna hii ya kufahamu kutoka RITA

Soma na hizi

Tupia Comments