AyoTV

Sababu za CHADEMA kwa nini fedha haipatikani mifukoni (+Video)

on

Leo July 31, 2017 Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kupitia Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe imekutana na Waandishia wa Habari katika mkutano uliofanyika Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, CHADEMA imetoa taarifa ya maazimio baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho kukutana kwa siku mbili mfululizo July 29-30, 2017 katika Hotel ya Double Tree, Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zao.

Akizungumzia hali ya Uchumi Mbowe amesema hali ya ujazo wa fedha imekuwa kinyume na ilivyokuwa 2015 kwani imeathiri biashara, uzalishaji na thamani ya Mali:>>>”Mzunguko wa fedha kwa mwaka inaonesha May 2015 iliongezeka kwa asilimia 15.2 wakati May 2017 ilikuwa na ongezeko hasi kwa asilimia -3. Hiki ni kielelezo cha usimamizi hafifu wa uchumi na ndio msingi wa ukata unaondelea nchini.” – Freeman Mbowe.

ULIPITWA? CHADEMA kuhusu hali ya Uchumi wa nchi, imetaja vigezo 5…play kwenye video hii kutazama!

Soma na hizi

Tupia Comments