AyoTV

Anayedaiwa kumhonga Waziri Lukuvi Milioni 90 alivyoachiwa huru (+video)

on

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuachia huru, Mohamed Kiluwa (50) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa sababu ushahidi wa mashtaka haukujitosheleza.

Pia mahakama hiyo imeamuru fedha zake ambazo ni Milioni 90 anazodaiwa kutaka atoe rushwa arudishiwe. Kiluwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone ameachiwa huru na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Samweli Obas.

“Kwa mantiki hiyo ushahidi ulioletwa haukuitosheleza mahakama, hivyo inamuachia huru na fedha alizokuwa nazo Milioni 90 arudishiwe,”.

Awali katika hukumu hiyo, Hakimu Obas amesema mlalamikaji aliieleza mahakama kuwa hati za Kiluwa zimepatikana kihalali, hivyo anakiri zilitolewa kihalali. Pia msiri wake alimwambia mshtakiwa atamletea Dola Elfu 50 ila zilizokamatwa ni Dola 40, jambo ambalo mahakama inatilia mashaka.

Pia amesema kielelezo cha CD kina mashaka kwa sababu kina mapungufu ambapo ukiisikiliza mwanzo hadi mwisho wa CD hakuna kauli ambayo ameitoa mshtakiwa akisema anatoa Dola Elfu 40.

Katika kesi hiyo Kiluwa anadaiwa kuwa July 16, 2018 kati ya saa 6 na saa 8 mchana akiwa Mkurugenzi wa kampuni hizo mbili alitoa rushwa ya Dola za Marekani 40,000 ambazo ni sawa na Sh. milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.

Mshitakiwa anadaiwa kutoa fedha hizo kwa lengo la kwamba asiwasilishe hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura kilichopo eneo la viwanda lililopo Kibaha mkoani Pwani.

BREAKING: Tajiri Kiluwa aachiwa huru mahakamani, Mwanae aangua kilio

Soma na hizi

Tupia Comments