Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na muwekezaji Aliko Dangote Ikulu DSM
Share
Notification Show More
Latest News
Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’
June 2, 2023
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
June 2, 2023
Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano
June 2, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na muwekezaji Aliko Dangote Ikulu DSM
Top Stories

Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na muwekezaji Aliko Dangote Ikulu DSM

December 10, 2016
Share
3 Min Read
SHARE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu  ambao  walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.

”Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ” – Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia  kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43  kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora  kuliko kuagiza nje.

Katika kuthibitisha hilo,  tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi  ambazo zinapatikana nchini.

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya  Tanzania  na kamwe hana  nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

VIDEO: Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kufungwa kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote

You Might Also Like

Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’

Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano

Amnesty yaonya Iran dhidi ya Kunyonga kwa Kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya

TAGGED: Dk. Magufuli, DONGOTE, John Magufuli
Admin December 10, 2016
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Nyingine ya Mchungaji anayewanywesha waumini dawa ya kuua bakteria “Dettol”
Next Article PICHA 8: Christopher Ole Sendeka na viongozi wengine walivyoapishwa na Rais JPM leo IKulu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’
Top Stories June 2, 2023
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
Top Stories June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
Top Stories June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
Sports June 2, 2023

You Might also Like

Top Stories

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

June 2, 2023
Top Stories

Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano

June 2, 2023
Top Stories

Amnesty yaonya Iran dhidi ya Kunyonga kwa Kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya

June 2, 2023
Top Stories

Elon Musk kwa mara nyingine tena ndiye mtu tajiri zaidi duniani

June 2, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?