Michezo

Alipoulizwa Moyes kuhusu kumpa Rooney unahodha wa Man United

on

article-0-1B20F53D00000578-429_634x521

Baada ya nahodha wa sasa wa klabu ya Manchester United Nemanja Vidic kutangaza kwamba ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, kumekuwepo na mjadala katika vyombo vya habari kuhusu mchezaji gani anayefaa kuirithi nafasi yake ndani ya klabu hiyo.

Mmoja wa wachezaji anayepewa nafasi kubwa ni mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney ambapo kwenye mkutano na waandishi wa habari kocha David Moyes aliulizwa kuhusu mjadala huo na kusema ‘tunataka mtu ambaye ataonesha sifa za kuwa kiongozi, sio tu uwanjani bali pia nje ya dimba…. ni kitu kikubwa kuwa nahodha wa Manchester United.

‘Mtu ambae anatakiwa kuwa nahodha anapaswa kujua nini inaamanisha kuwa kiongozi ndani ya klabu hii, majukumu ambayo nahodha anatakiwa kuwa nayo, nadhani tuna wachezaji wengi wanaoweza kushika nafasi hiyo na watapata nafasi hiyo ikiwa mmoja wao atakidhi vigezo’

Alipoulizwa moja kwa moja kwamba Rooney anaweza kupewa nafasi hiyo meneja huyo wa United aliongeza: “kama nilivyosema, nitampa kila mtu nafasi ya kuonyesha kama anafaa kuwa nahodha katika miezi kadhaa inayokuja” 

 

Tupia Comments