Simon John Mseke ndio jina lake na ana umri wa miaka 49, bado anaonekana ni kijana na akisimama na watoto wake usipoambiwa unaweza kudhani ni watu na kaka yao lakini ukweli ni kwamba huyu ndio baba mzazi.
Anasema alioa mapema sana kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 18 ambapo akiwa na miaka 19 ndio alizaliwa staa wa hiphop Joh Makini ambae ameanza kumiliki headlines za bongo kwa uzito zaidi ya miaka mitano iliyopita.
Simon ambae ni mfanyabiashara wa madini anasema ‘muziki wao kwa kweli ni biashara, muziki una faida kubwa sana kwao Joh Makini na Nikki wa II na ninawaombea Mungu wazidi kufanya vizuri zaidi, kwa kweli wamefanya vitu vingi sana vingine siwezi kuvikumbuka kwa sasa ila tayari wamenunua viwanja hapahapa Arusha na wala sio kiwanja kimoja wala viwili’
‘Joh tabia yake ni ya upole toka mdogo na sio muongeaji tofauti na Nikki…. walipoanza muziki sikujua ila nilikuja kuwakutia tu kwenye mtiririko kama Joh alianza akiwa shuleni tu na alikua anatungatunga nyimbo zake hapa nyumbani vivyo hivyo kwa Nikki wa II, sikuwahi kufikiria kuwakataza kwa sababu sikuwahi kufikiria kama ni kitu kibaya’
Mzee anasema ‘mimi nasikiliza sana hiphop wala sio kitu ya kuuliza, nyimbo zao ninazozipenda ziko nyingi na nyingine hazijatoka hata redioni… ila napenda Pea, bei ya mkaa na bye bye’
millardayo.com : kuna nyimbo gani nyingine za hiphop Tanzania unazisikiliza?
John Simon: ‘Sijui utasema nawapendelea, nasikiliza zao tu na G Nako na Lord Eyez ndio cd nilizonazo hapa’