Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Habari za Mastaa

KESI YA WEMA:MAHAKAMA YAMPA MASHARTI KUHUSU INSTAGRAM YAKE

on

Msanii wa Filamu, Wema Sepetu amesomewa kosa moja la kuchapisha video yake ya picha ya ngono kupitia kurasa yake ya Instagram katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wema amesomewa kosa hilo na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi, Maila Kasonde.

Wakili Kombakono amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la kuchapisha picha za ngono kinyume na sheria.

Anadaiwa ametenda kosa hilo, October 15, 2018 katika sehemu tofauti tofauti ambapo alichapisha kupitia mtandao wake wa Instagram video yake ya picha za kingono kitu ambacho hakiruhusiwi

Baada ya kusomewa kosa hilo, Hakimu Kasonde alimuuliza Wema,

HAKIMU: Mshtakiwa umesikia mashtaka yako ?

WEMA: Ndio

HAKIMU: Ni kweli ulichapisha hizo taarifa kupitia Instagram yako ?

WEMA: Sio kweli.

Baada ya kukana wakili wa utetezi, Semwanza Rubeni alimuombea dhamana mteja wake.Hakimu Kasonde amesema anatoa masharti ya dhamana ambapo Wema anatakiwa asaini Bondi ya Shilingi Milioni 10 na awe na mdhamini mmoja atakayesaini kiasi hicho.

Pia amesema anatakiwa asiweke picha yoyote ya Porno ‘Ngono’ kwenye mtandao wake wa Instagram wala maneno yenye uelekeo ama viashiria vya Kingono.Wema kaachiwa kwa dhamana, kesi imeahirishwa hadi November 11,2018.

BREAKING NEWS: Wema Sepetu afikishwa Mahakamani Kisutu

Soma na hizi

Tupia Comments