AyoTV

Samson kaamua kudili na kuuza Mbwa tu na hakosi Milioni kwa mwezi Mwanza

on

Inaweza kuwa nadra kusikia mtu akikwambia anataka kuanza biashara ya kuuza Mbwa ila ni biashara ambayo inafanywa na watu wachache na hawakosi senti zao.

AyoTV inakukutanisha na Samson Magoli ambaye ni mkazi wa Mwanza, huingiza sio chini ya shilingi milioni mbili kwa mwezi na alianza kwanza kwa kuwapenda Mbwa na ni zaidi ya miaka mitatu toka aianze hii biashara.

Mbwa wake wa kwanza kumuuza pesa nyingi alimuuza kwa shilingi milioni moja na laki nne, wengine kwa mwaka huu amekua akiwauza kwa shilingi laki moja na nusu mpaka laki mbili, zaidi unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini.

VIDEO: Binti Mtanzania wa miaka 20 aliyelipwa BILIONI 1 Marekani kwa dili moja, tazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments