Msanii Bobi Wine wa Uganda ambaye pia ni mbunge amepewa sapoti na wasanii wenzake baada ya kuungana kwa pamoja kufuatia kukamatwa kwake, Bobi Wine ambaye ni Mbunge wa Kyadondo amekamatwa siku kadhaa zilizopita baada ya dereva wake kuuawa kwa kupigwa risasi.
Tukio hilo lilitokea August 13, 2018 baada ya gari lililokuwa kwenye msafara wa Rais Museveni kushambuliwa katika mji wa Arua, hivyo kupelekea Bobi Wine kukamatwa ikiwa dereva wake amepigwa risasi na kuuwawa.
Awali iliripotiwa kuwa Bobi Wine amekamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za makosa ya uhaini lakini leo mtandao wa BBC umesema kuwa msanii huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa mawili la kumiliki silaha kinyume cha sheria na shitaka moja la kupatikana na sílaha.
Hiyo ni baada ya Bobi Wine kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi nchini Uganda katika Mji wa Gulu, kama utakuwa unakumbuka vizuri kufuatia kuuwawa kwa dereva wake, Bobi Wine aliandika kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa dereva wake ameuawa na Polisi wakidhani kuwa ni yeye alikuwa akiendesha gari hilo.
Dereva wa msanii na mbunge Bobi Wine amepigwa risasi