Habari za Mastaa

Chris Brown baada ya kukosa tuzo ‘BET’

on

Hii ni nyingine ya kuifahamu kutoka Marekani kuhusiana na staa maarufu Chris Brown ambaye amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na caption yake ambayo  imehusishwa na tuzo za BET zilizofanyika June 25,2018.

Chris Brown amepitisha miaka mitatu mfululizo bila kushinda tuzo za BET ikiwa 2016,2017 hakushinda na mwaka huu 2018 alitajwa kwenye vipengele viwili Best Male RnB/Pop Artist na Video Director of the year na hajaibuka mshindi.

Kupitia instagram account Chris Brown ameandika “Sihitaji tuzo ili niwe mfalme” ambapo caption hiyo inahusishwa kuwa imemchukiza staa huyo kutokana na kufanya kazi kwa bidii lakini haibuki mshindi.

Uwoya kafunguka tusiyoyajua “Nimepiga picha na Mama Mkwe, Dogo Janja nimemzidi vingi”

Soma na hizi

Tupia Comments