Premier Bet SwahiliFlix Ad Vodacom Ad

Habari za Mastaa

MC Pilipili -“Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa”

on

Mchekeshaji Mc Pilipili amefanya mahojiano na kipindi cha radio cha Clouds FM cha Leo Tena na amezungumza kuhusiana na vitu vingi vinavyomuhusu mpenzi wake Phelomena ikiwemo na kiasi alichokitoa kwaajili ya mahari.

>>>”Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa”

>>>‘’Ni kweli nimeokoka, ndio maana kwenye sherehe ya kuvishana pete hakukuwa na vinywaji vikali, hatuishi pamoja na mpenzi wangu ila huwa anakuja nyumbani kwangu kupika’’

>>>‘’Mshenga aliniambia mahari ni Mill. nane, na tulifanya mazungumzo kidogo, hivyo hadi sasa nimetoa mill. tano bado mill. mbili ’’

>>>Mpenzi wa Mc Pilipili Phelomena amesema mume wake mtarajiwa sio dhaifu kama watu wanavyodai baada kutoa machozi siku ya kuvishana pete.
‘’Hata mimi imeni’challenge’ sana nilisikia viabaya sana Mc pilipili sio dhaifu kama angekuwa dhaifu nisingekuwa naye napenda mwaunaume anayenikoromea’’

>>>‘’Unajua kwenye mahusiano yetu, maneno mengi yalizungumza kuwa mimi ni muongo na haitowezekana kumvisha pete mpenzi wangu, wengi walikuwa wakisema mahusiano yangu yatafikia wiki mbili yatavunjika, wengi walikuwa hawaamini kama nitatoa mahali na nitafikia hatua ile, nilikuwa napata wasichana waliokuwa hawana vitu ninavyovipenda lakini huyu ana vitu ninavyovipenda, ni msichana ambaye tuliandamwa na watu waliokuwa wakileta maneno kuwa msichana huyo ametoka na wanaume wengi, sikuyafuatilia’’

NISHA BEBE KAWAFUNGUKIA NI KUHUSU VIBENTEN

Soma na hizi

Tupia Comments