Habari za Mastaa

Nisha Bebe aamini aliko kama kuna mapenzi ya dhati

By

on

Muigizaji na msanii wa Bongo Fleva Nisha Bebe hatimaye ameamua kumuweka wazi mpenzi wa sasa hii ni baada ya kuficha kwa muda mrefu kuhusiana na mahusiano yake ambapo amekuwa mgumu kuelezea uhusiano wake mpya.

Kupita ukurasa wake wa instagram amemuonyesha mwanaume huyo mwenye asili ya kizungu na kusema kuwa kwa sasa hapo ndipo moyo wake ulipo ingawa alishawahi kujihusisha kimapenzi na Wafrika, Waarabu lakini anaamini kuwa wazungu ndio wanamapenzi ya kweli.

“Ni ngumu sana kuficha hisia zangu kwa mtu nnayempenda nimeshakuwa na mblack, mwarabu ila kote niliambulia usaliti na uongo wa mapenzi. niliwahi sikia wazungu wana mapenzi ya kweli kuliko waafrica.. kujaribu si mbaya. me ni msafiri sijafika bado na M’Mungu anajua kama hapa ndo mwisho wa safari yangu au inaendelea kikubwa NIMESHAMPATA NA MANENO SIJALI”

Hatimae Moni na Nai watoka pamoja, wakiri kurudiana

Soma na hizi

Tupia Comments