Habari za Mastaa

Nandy -“Mimi na Ruby sio marafiki, hatuongei” (+video)

on

Mwimbaji Nandy ‘African Princess’ amefunguka kuhusu uhusiano alionao na mwimbaji mwenzake Ruby baada ya kuhusishwa kuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu huku chanzo cha ugomvi huo ukitajwa ni mafanikio ndani ya muziki.

Nandy ameyaongea hayo katika mahojiano aliyoyafanya na mtangazaji Mzazi Mtuva katika kipindi cha Mseto East Afrika akiwa nchini Kenya alipokwenda kutambulisha ngoma yake mpya ya ‘Hazipo’.

“Mimi na Ruby hatuongei, sio marafiki , sijui mara ya mwisho nimemuona mwaka jana mwezi wa ngapi, hatuonani lakini tuko poa, tukikutana tunasalimiana mambo vipi/freshy ugomvi wa management upo kwenye moyo wake sidhani kama nahusika sana Ruby na kuondoka ” >>> Nandy

BARNABA KASHINDWA KUKAA NALO MOYONI, KASHARE FURAHA YAKE NA MASHABIKI

Soma na hizi

Tupia Comments