Habari za Mastaa

Cheki toleo jipya la viatu vya Yeezy, Kanye West katuonyesha

on

Tolea jipya la viatu aina ya Yeezy vimetoka ambavyo ni “Yeezy 700 V3” kupitia ukurasa wa twitter wa Kanye West ametujulisha  kuhusu ujio huo ikiwa ni muendelezo wa viatu hivyo ikishirikiana na kampuni ya Adidas.

Jumatatu ya August 20,2018 Kanye West alitangaza punguzo la bei katika tolea la Yeezy 350 V2 kupitia ukurasa wake wa twitter na kusema kuwa litafanyika Septembe 21,2018 na pia aliongeza kwa kusema amekuwa akifanya utengenezaji huu wa viatu hivyo anatamani watu wengi wawe na uwezo wa kuvimiliki na ndio maana ameamua kufanya punguzo la bei.

Tarehe rasmi ya toleo jipya la viatu  vya Yeezy 700 V3 haijawekwa wazi lakini taarifa zinadai kuwa Yeezy 700 V2 ndio itatangulia kuanza kutolewa huku toleo la Yeezy 700 V3 itatolewa 2019 na utofauti mkubwa uliopo kati ya V2 na V3 ni soli ya viatu hivyo.

African Rally Championship 2018 imerudi tena

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments