Top Stories

HEKAHEKA: Mwenyekiti atuhumiwa kuua kwa kutumia nyundo DSM

on

Hekaheka ya leo March 14, 2018 imetokea Keko ambapo inamuhusu Mwenyekiti anayetuhumiwa kuua baada ya kumpiga mtoto wa mtaani kwake na nyundo na kumkata kata viungo na kusababisha umauti huku ikidaiwa kuwa kijana huyo ni mwizi.

Mama wa mtoto ameeleza kuwa alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mwanae anapigwa na hata kama atapona atakuwa hana mikono na miguu lakini alipouliza nani kampiga wakasema Mwenyekiti, mama huyo akasema kuwa kisa hakijui ila kazi anayoijua ya mwanae nikugonga sofa.

Kwa upande wa Mwenyekiti ambaye majina yake ni Ismail Yusuph amesema kwanza yeye watu wanamuamini kwa kuwa ni mtu anaye chukia uhalifu lakini suala la kuua anasema angeua asingekuwa mtaani anakunywa kahawa lakini anasema alipata taarifa ya kijana kaiba ndipo alipoenda..

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza STORY KAMILI

HEKAHEKA: Chatu asababisha Wanaume kulala nje ya ndoa zao DSM

Tunda na Casto Dickson wamezungumza “Tukiwa wapenzi kuna ubaya gani?”

Soma na hizi

Tupia Comments