Top Stories

HEKAHEKA: Chatu asababisha Wanaume kulala nje ya ndoa zao DSM

on

Hekaheka ya Leo March 5, 2018 imetokea Mbezi Msigani jijini Dar es Salaam ambapo nyoka mkubwa aina ya Chatu ameleta taharuki ambapo imeelezwa kuwa amesababisha wakazi wa eneo hilo kulala mapema na wengine kulala nje ya ndoa zao kwa kuhofia kumezwa inapofika usiku.

Wakazi wa Mbezi wamesema wamemuona ni chatu mkubwa ambae amewafanya kuwa waoga, taarifa pia zilimfikia Mwenyekiti wa Shina ambaye amethibitisha hilo na kusema kwamba walitoa taarifa Polisi na kisha baadae wakapeleka taarifa kwa Maliasili.

Bonyeza PLAY hapa kusikiliza FULL STORY

HEKAHEKA: Mwanaume aelezea jinsi Mkewe alivyopotea na kukuta mwili wake umeliwa

Soma na hizi

Tupia Comments