Top Stories

Mwalimu Mkuu anayevaa sare sawa na Wanafunzi wiki nzima

on

Leo June 5, 2018 Nakusogezea stori kumhusu Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Friends School Kamusinga nchini Kenya  Alex Maina Kariuki amewashangaza wengi kwa tabia yake ya kuvaa sare za wanazovaa wanafunzi jumatatu mpaka ijumaa.

Duru za kuaminika zimeeleza kuwa mwalimu huyo anafanya hivyo ili kupima ubora wa sare wanazogawiwa wanafunzi, pili kutaka kuwa karibu na wanafunzi lakini sababu kubwa zaidi ikitajwa kuwa kutaka kuwaonesha wanafunzi kuwa Mwalimu Mkuu ni binadamu wa kawaida tu kama wao.

Aidha utamaduni huo wa Mwalimu Mkuu umekuwa ukileta changamoto nyakati fulani kwa waalimu na wanafunzi pale wanapodhani kuwa Kariuki naye ni mwanafunzi kumbe siyo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa utamaduni huo wa mwalimu mkuu haujaanzia katika shule hiyo bali amekuwa akifanya hivyo toka shule aliyotoka.

Naibu Waziri alivyocheza na nyoka bila woga.

Soma na hizi

Tupia Comments