Michezo

Sababu za wachezaji wa Leganes kuvaa jezi zenye majina ya mama zao

on

Wachezaji wa club ya Leganes ya Hispania weekend iliyomalizika siku ya Jumamosi ya March 9 2019 wameungana na watu mbalimbali duniani kote kusherehekea siku ya kimataifa ya wanawake Duniani (Women’s International Day).

Wachezaji wa Leganes wakicheza katika game ya LaLiga dhidi ya Atletico Madrid siku ya Jumamosi ya March 9 ikiwa imepita siku moja ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka March 8, waliingia katika mchezo huo wakiwa wamevaa jezi zenye majina ya mama zao kama ishara ya kusherehekea nao siku yao.

Siku ya wanawake duniani imelenga kutambua na kupambania haki za msingi za wanawake, hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa Leganes iliyo nafasi 13 katika msimamo wa LaLiga kupoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Saul Niguez dakika ya 50.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments