Habari za Mastaa

DAH!! AKA ajuta kuachana na mzazi mwenzake

on

Staa wa rap kutokea Afrika Kusini AKA ameamua kufunguka kupitia twitter account yake machungu anayoyapitia baada ya kuachana na mzazi mwenzake Zinhle na kuanzisha mahusiano mapya na mtangazaji Bonang mwaka 2015.

Kupitia twitter account ya rapper huyo ameandika “Nilisaliti familia yangu kwaajili ya kusalitiwa, haya ni malipizi”

AKA pamoja na Bonang waliweka mahusiano yao wazi mwaka 2015 baada ya rappa huyo kuachana na mazazi mwenzake kipindi akiwa mjamzito na tetesi kudai kuwa Bonang na AKA wameachana mwanzoni mwa February mwaka huu 2018.

AKA kwa sasa ana mtoto mmoja na aliyekuwa mzazi mwenzake Zinhle na kupitia maneno ya kwenye twitter account yake anaonekana kuumizwa na maamuzi aliyoyafanya.

1.Bonang na AKA

2.AKA na mzazi mwenzake Zinhle

Matokeo ya Mtoto aliyemshtaki Baba yake yametoka, anazungumza Kiingereza

 

Soma na hizi

Tupia Comments