Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Club ya soka ya Simba Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu, leo August 7, 2017 imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeahirishwa hadi August 16, 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na Wakili wa Serikali, Elia Athanas ambaye amedai Mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba ipangiwe tarehe nyingine ambapo Hakimu Mwambapa aliahirsha kesi hiyo hadi August 16, 2017.
VIDEO: Rais Magufuli afunguka kuhusu kutawala miaka 20, play hapa chini kumtazama