Habari za Mastaa

Taarifa ya kulazwa kwa Rick Ross yazidi kuwagusa Mastaa

on

Msanii wa Muziki wa Hip Hop nchini Marekani mwenye umri wa miaka 42 Rick Ross amelazwa katika hospitali iliyopo Miami, huku taarifa zikiwa bado hazijathibitisha kuwa ni ugonjwa gani unaomsumbua bali imeelezwa kwamba yupo katika hali mahututi.

Sasa katika Mitandao ya kijamii wasanii mbalimbali wameendelea kuguswa ambapo baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Snoop ambaye aliandika kwenye twitter...>>>”Maombi kwa wingi kwa rafiki yangu Rick Ross”, “Tunatumai utapona ndugu yangu.”

Pamoja na hivyo Familia ya Rick Ross imekana taarifa kwamba mwanamuziki huyo amewekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

BLACK & WHITE: Lulu Diva awalipia viingilio Mashabiki zake

ON AIR: “Bora zamani, sasa hivi ndio sina ushikaji kabisa na Nandy” – BILNAS

Soma na hizi

Tupia Comments