AyoTV

Miss Tanzania ajitetea kushindwa Miss World “Nchi yangu haikutimiza wajibu wao” (+video)

on

Miss Tanzania, Queen Elizabeth Makune amefunguka sababu za kushindwa kuchukua taji la Miss World mwaka 2018 lililofanyika Sanya nchini China ambapo amesema jukumu kubwa lilibaki kwa nchi yake.

Akizungumza na vyombo vya habari, Queen Elizabeth amesema nchi nyingine zimewekeza kwenye mashindano hayo kuanzia ngazi ya serikali hadi sehemu nyingine kwani kushinda Miss World hakutegemei uzuri wa mtu bali ushiriki wa nchi yake.

“Nakumbuka nilishasema wakati naenda kushiriki kwamba kushinda Miss World sio kitu nachofanya peke yangu bali tunaingia nchi kama nchi na tunapambana, nimefanya kwa juhudi zangu zote, hivyo jukumu lilibaki kwa serikali na Watanzania“amesema.

TABU WANAYO KUTANA NAYO WASAFIRI STENDI UBUNGO

Soma na hizi

Tupia Comments