Club ya Man City leo Alhamisi ya February 28 2019 imetangaza kupata dili kubwa kutoka kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma, Man City sasa imeripotiwa kuwa itaachana na kutumia vifaa vya Nike baada ya kuingia mkataba mkubwa na Puma utakaowafanya walipwe mkwanja mrefu kwa mwaka ukilinganisha na Nike walivyokuwa wanawalipa.
Mkataba wa Nike na Man City unamalizika mwisho wa msimu huu na Puma ndio wameshinda dhabuni ya kuitengenezea Man City vifaa vya michezo kwa msimu ujao, hiyo ni baada ya kuipiku Nike katika tenda kwa dau nono walilopata.
Imethibitika kuwa Puma wameingia mkataba wa miaka 10 na Man City wa kuwatengenezea vifaa, mkataba ambao una thamani ya pound milioni 650 ambazo ni zaidi ya Trioni 2 za Tanzania, hivyo ni sawa na Man City kuwa watakuwa wanalipwa pound milioni 65 kila mwaka, Man United wakiendelea kuongoza kwa kuwa wanalipwa pound milioni 75 na Adidas kwa mwaka na Chelsea pound milioni 60 kwa mwaka kutoka Adidas.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake