Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Habari za Mastaa

Ommy Dimpoz afanyiwa operesheni ya Koo

on

Ommy Dimpoz ni miongoni mwa mastaa ambao wamezoeleka kuonekana kupost picha na videos katika mtandao wa instagram kila mara, lakini kwa wiki kadhaa Ommy Dimpoz ameonekana akiwa kimya katika ukurasa huo na mashabiki kubaki na maswali.

Leo June 15,2018 kupitia ukurasa wa instagram wa Ommy Dimpoz ameelezea chanzo cha ukimya wake na kusema kuwa alikuwa nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa katika matibabu ya takribani siku 15 na kufanyiwa opereshani ya koo.

Katika mazungumzo aliyoyafanya na mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram hajaelezea sababu ya opereshani hiyo aliyofanyiwa nchini Afrika KusiniĀ na kusema kuwa kwa sasa yupo kwenye mapumziko.

šŸ™ā¤ļø

A post shared by Ommy Dimpoz (@ommydimpoz) on

EXCLUSIVE: Mama Hamisa kazungumza “Namwambiaga Hamisa akipata mimba asitoe”

 

Soma na hizi

Tupia Comments