Top Stories

Mwaliko aliopewa Rais Magufuli kutokea kwa Mufti Mkuu Tanzania

on

Rais wa Tanzania,John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Sherehe za Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W), ambazo zinatarajiwa kufanyika November 20, 2018.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubairy bin Ally, amewaambia waandishi wa habari kuwa kabla ya kufanyika kwa sherehe za Baraza hilo, kutatanguliwa na sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W) ambazo zitafanyika November 19, 2018.

Pia Mufti Zubairy bin Ally, amesema katika sherehe hizo itakuwa ni fursa tosha ya kuzungumzia suala la mmomonyoko wa maadili ikiwemo suala la Ushoga ambalo hivi karibuni limeibua mijadala katika maeneo mbalimbali.
SAKATA LA USHOGA: MUFTI MKUU WA TANZANIA ATOA KAULI ‘MUNGU ALIANGAMIZA KIJIJI’

Soma na hizi

Tupia Comments