Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

fB insta twitter

Hii ni tweet ya Fid Q kuhusu Francis Cheka kuhukumiwa miaka mitatu jela?

on

Tweet 2February 2 2015 bondia Mtanzania Francis Cheka alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani pamoja na faini aliyoitaja kuwa milioni moja na laki sita baada ya kupatikana na kosa la kumpiga meneja aliekua amemuajiri kwenye Bar yake Morogoro.

Ni hukumu ambayo kila mmoja ameipokea kwa muonekano wake ambapo japo Rapper Fid Q hakumtaja mtu kwenye tweet hiyo, imeonekana kama inahusu kilichomtokea Francis Cheka ambacho kimejadiliwa na watu mbalimbali kwenye twitter wiki hii.

Fid aliandika ‘Una muajiri mtu kwa nia nzuri, yeye anakuibia na ukimuhoji anakupa majibu ya dharau wakati anajua wewe ni mbabe, na ukimdunda unaswekwa jela’

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter,  Instagram,  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments