Michezo

Ni kweli David Luiz hakupatana na Mourinho? mazungumzo yao ya kwenye simu je?

on

LuizMbrazil David Luiz ni staa wa soka ambae tunafahamu kabla ya kujiunga na PSG ya Ufaransa alikua anaichezea Chelsea toka mwaka 2011.

Kumekua na stori nyingi zinaandikwa kwamba mkali huyu aliondoka Chelsea sababu ya kuwa na ugomvi au kutopatana na kocha Jose Mourinho.

Namnukuu akisema >>> ‘Niliamua kuondoka baada ya msimu kuisha, Chelsea walinishawishi kusaini mkataba mpya lakini nikawaambia sasa hivi sina furaha na Chelsea kama ilivyokua kwenye miaka iliyopita, nilikua na uhusiano mzuri na Wachezaji wenzangu na kila mtu kwenye club lakini pia nilifanya maamuzi ya kuondoka kwenye kujaribu sehemu nyingine’

Watu wanajaribu kutengeneza stori za ugomvi kati yangu na Mourinho lakini ukweli ni kwamba hatujawahi kuwa na uhusiano mbaya, wakati mwingi alipokua hanipi nafasi ya kucheza walisema nina tatizo nae, haikuwa kweli….. ‘ – David Luiz

Kwenye sentensi ya mwisho mtoto huyu wa Mwalimu amesema ‘Wakati naondoka Chelsea Mourinho hakufanya jitihada za kunibakisha, nilisema sijisikii vizuri Chelsea hivyo nataka kuondoka…. hakufanya jitihada sana, nilikua Brazil wakati huo kwenye kombe la dunia, niliongea nae kwenye simu kuhusu kuondoka na nakumbuka aliniambia tu ‘OK, UNAWEZA KWENDA’

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram,  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments