Leo November 25, 2016 ndani ya XXL ya Clouds FM kulikuwa na Exclusive Interview na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG) Ruge Mutahaba ambapo amezungumzia mambo kadhaa ambayo yalikuwa na maswali mengi mtaani.
Miongoni mwa vitu Ruge amevitolea ufafanuzi ni pamoja na kinachozungumzwa mitaani kwamba kuna wasanii ambao ametofautiana nao na amesimamisha nyimbo zao kuchezwa Clouds kitu ambacho Ruge amesema yeye binafsi hana tofauti na msanii yeyote isipokuwa wasanii wanaotofautiana na taasisi ya Clouds Media kinachofanyika ni kufata sheria za kampuni tu.
Pia kuna tatizo la uchache wa tuzo za wasanii Tanzania kitu ambacho amesema Baraza la Sanaa la Taifa BASATA linachangia kudidimiza hatua za sanaa kwa kuzuia wadau kuanzisha tuzo nyingine, pia utaratibu wa kufungia Video zao linatengeneza umaarufu wa wasanii na video zao badala ya kuboresha kama wanavyotaka wao.
Mengine aliyozungumza Ruge Mutahaba nimekuwekea hapa. Full Interview ipo chini
'Mwaka kesho FIESTA itakua mapambano maana hatutaleta msanii wa kimataifa, tutawalipa zaidi Wasanii wa TZ lakini watakua na deni'-Ruge #XXL pic.twitter.com/2sImm0SIhu
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Hela nyingi tulizowapa wa kimataifa zimetupa hasira tuweke bidii na kusema mwaka kesho FIESTA hatutataka Msanii wa kimataifa'-Ruge #XXL pic.twitter.com/xpDa3eoXm4
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'TZ ilitakiwa kuwa na matukio ya utoaji TUZO angalau 5 tofauti kwa mwaka lakini kumekua na mlolongo wa kibali kwa wanaotaka kuandaa'- RUGE pic.twitter.com/PPQlNE4XFl
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Diamond anajua ana muda wake ndio maana anatengeneza CHIBU PERFUME, anajua hata akishuka ana vitu vyake vitamsaidia' – Ruge #XXLcloudsFM pic.twitter.com/u2o4pE8bdP
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Wasanii wanaolalamika ni wale wanaoshuka kimuziki na hawakujiandaa kimaisha, waliojiandaa kimaisha huwa hawalalamiki' – Ruge #XXLcloudsFM pic.twitter.com/R4cevX9FQF
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'La T.I.D… CloudsFM haina studio, naanzia wapi kulizungumzia…. tunapenda mitandao mno na tunapeleka vitu huko, Mahakama ipo' – Ruge #XXL pic.twitter.com/P5X2EJynWA
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Mimi Ruge Mutahaba ndio nimeandika nyimbo za Ruby pia 'Na Yule' niliandika na Barnaba, 'sijutii' na 'forever' zote hizo' – Ruge #XXL pic.twitter.com/dShRytPrR0
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Kuna Wasanii Clouds imefungia nyimbo zao lakini mimi binafsi nazipenda na ninazisikiliza kila siku, napenda nyimbo za Rama Dee' – Ruge #XXL pic.twitter.com/4JPUd1pvrr
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Ya Jaydee tulienda Mahakamani na alishindwa kuthibitisha kama ni kweli, tulishinda kesi.. imeonyesha tusituhumu kama hatuna uhakika'-RUGE pic.twitter.com/h41PFMsvGp
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
B12: 'Mkikutana na Jaydee uko tayari kuyamaliza mnywe Kahawa?'
RUGE: 'Hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko' pic.twitter.com/wu9LBsmubE
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Tulimaliza ila tunasubiri oda maana tuliambiwa tusipige nyimbo wala kutaja jina lake, labda tukikutana nimuombe kama tutaruhusiwa' -RUGE pic.twitter.com/OiQOwkMcoi
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
Mimi naamini sana kwenye kipaji, Mungu anatoa kipaji. Sikumbuki kama kuna mtangazaji niliwahi kumuajiri kwa kuangalia CV #RugeMutahaba #XXL pic.twitter.com/dHrEVzJvdN
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
Diamond Platnumz aliwahi kupigwa chini alipotaka kujiunga na nyumba ya vipaji Tanzania THT lakini hakukata tamaa.-Ruge Mutahaba #XXLcloudsFM pic.twitter.com/x9iKGGvIQA
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Wasanii wa Hiphop TZ ndio wajiulize wanampango gani na Hiphop, naona kama wameichukulia poa, nataka watengeneze utofauti wa kibiashara' pic.twitter.com/SsgiupziAy
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Beef za kijinga zisizokua na tija na hela hazina maana, beef za kibiashara zitazojaza uwanja na kuleta hela sina neno nazo' – RUGE #XXL pic.twitter.com/5qEQEvmKnr
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
VIDEO: Yapo hapa aliyoyasema Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group kuhusu Muziki, Tuzo, Beef na Wasanii, FIESTA2017.