Stori Kubwa

Mwanza nzima hili ndio litakua gorofa refu kuliko yote 2016.

on

333Mwanza ni moja ya sehemu tatu za Tanzania ambazo huwa nazipenda sana na hata wakati mwingine kuvutiwa kuzitembelea kila ninapopata nafasi.

Mabadiliko ambayo wengi wangependa kuyaona ni jiji hili lilibarikiwa kwa kupewa pia ziwa Victoria, liendelee kupendeza kihalali kutokana na mpangilio unavyohitajika.

2Hili jengo linajengwa maeneo ya Capri Point ambapo ni jengo la Hoteli litakalokuwa na gorofa kumi na tano, ni jengo la hoteli ambayo ni ya Nyota tano itakayokuwa karibu na vyumba mia mbili vya kulala.

3Limeanza kujengwa tangu November 2013 na linatarajiwa kumalizika mwaka 2016 huku gharama ya kulijenga ikiwa ni zaidi ya bilioni 72.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments