Maajabu

Mambo matano ya kufahamu kuhusu Mwanamke aliyemuuza mama yake mdogo Ruvuma.

on

kivuliUnaweza kujiuliza mara mbilimbili inakuaje mpaka mtu anapata ujasiri wa kumuuza mama yake mdogo? tena aliekamilika?

1. Mwanamke mwenyewe alieamua kumuuza mama yake mdogo, anaitwa Sophia Yasin Chambo (30) na ilikua February 17 2015 saa nane mchana maeneo ya Lizaboni, alikwenda nyumbani kwa Mfanyabiashara wa eneo hilo na kumwambia anahitaji kufanya nae biashara ili azidi kuwa tajiri.

2. Alimwambia anae mama yake mdogo na angehitaji kumuuza kwake ili amfanye kama zindiko biashara izidi kumuingizia pesa, alikubaliana kwamba atampeleka Mama mdogo akiwa kwenye gunia baada ya kumuua lakini Mfanyabiashara akasema anamtaka akiwa hai.

3. Walikubaliana bei ni Milioni 6.5 kutokea kwenye Milioni 10 aliyoanzia, kesho yake kweli Sophia alikwenda kumchukua mama yake mdogo aitwae Anita Kasim Mbawala mwenye umri wa miaka 40.

4. Unajua alimwambia nini mama Mdogo ili kumshawishi waende wote?? >>>> ‘Mama mdogo twende kuna sehemu Mwanaume amekupenda anataka kuishi na wewe, alikuona Iringa’ Mama mdogo akakataa na kusema hajawahi kuishi Iringa, baada ya kuona kagoma akamdanganya kuna watu wanataka akawafanyie kazi watamlipa vizuri sana ambapo mama mdogo alishawishika.

5. Walipofika Lizaboni kwa Mfanyabiashara Sophia alikamatwa sababu taarifa zilishawafikia Polisi tayari na mpaka sasa anaendelea kuhojiwa, upelelezi bado unaendelea na ukikamilika atafikishwa Mahakamani kutokana na biashara hii haramu ya kuuza binadamu.

Kusikiliza jinsi ilivyokuwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho bonyeza play kwenye hii sauti hapa chini…

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments