Ni baadhi ya majina ya sehemu ambazo zipo ndani ya mkoa wa Tanga (Clouds FM 96.0) ambapo hili la juu liitwalo Mkanyageni mwanzoni nilijiuliza maswali mengi sana na nikahisi vitu vingi na kutaka kujua ilikuaje?
Ukweli au maana ya hili neno mwenyeji wake aliniambia jina kamili la hii sehemu ni ‘Mkanyawageni’ miaka hiyo ya 70 na 80 kurudi chini liliitwa Mkanyawageni kwa sababu kila mgeni alieingia kuishi hapo ni lazima kwanza kabla ya kuendelea na maisha, alikua anatakiwa kukutana na Wazee/Wenyeji aonywe au kupewa maelekezo jinsi ya kuishi hapa.
Hakukua na chochote cha ajabu kwenye jinsi ya kuishi ndani ya hili eneo ila ulitakiwa kufata mambo yako tu, usifatilie wala kuingilia maisha ya yeyote hivyo kwenye miaka ya karibuni ndio wakaamua kulifupisha jina na kupaita Mkanyageni.
Ngomeni nilijaribu kupata Mwenyeji wa kunipa info lakini ikashindikana.
Chumvini ni eneo jingine lililofanya nisimame na kufatilia kujua ukweli wake, mmoja wa Wenyeji wa siku nyingi ameniambia jina hili lilitokana na eneo hili kuwa na ardhi yenye chumvichumvi.
Kange nako palinivutia nijue maana yake lakini sikufanikiwa, siku zote nimelisikia neno Kange kama aina ya chakula chenye aina yake ya upishi ambacho kinapatikana Dar es salaam sanasana kwenye bar.
Una sehemu yoyote ambayo unaijua na ina jina au majina yenye utata au yenye kufanya utake kujua nini maana yake? shea na mimi kwenye comment hapa chini mtu wangu, au nichek kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo, pia unaweza kunitumia kwenye mtuwakowanguvu@gmail.com