Mix

Hata kanda ya ziwa Airtel wamezisogeza Toyota IST, ni zamu ya mvuvi

on

Airtel MoneyMvuvi huyu anaitwa Kijiji Gweso anatokea wilaya ya Sengerema Mwanza na hapa ameichukua IST yake baada ya kuchukua ushindi wa Airtel Yatosha zaidi ambapo watu wa nguvu Jane Matinde (Afisa uhusiano wa Airet) na kaimu meneja mauzo kanda ya ziwa David Wankuru walikuwepo kufurahi nae na kumkabidhi.

SONY DSCKaimu Katibu wa Wilaya ya Sengerema Aaron L Laizer ( wa pili kushoto ndio alimkabithi Kijiji IST yake ambapo hakuchelewa kuyatoa ya moyoni baada ya kuichukua… >>> “Sijawahi kumiliki gari hivyo usafiri huu utanisaidia katika shughuli zangu za uvuvi, za kifamilia na kiuchumi kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwaambia watanzania wenzangu waamini kuwa Airtel inatoa magari na wao pia wanaweza kuibuka washindi.  Nawashukuru sana Airtel
kwa kuboresha maisha yangu na yawatanzania wengine walioshinda kama mimi”

SONY DSC

a3Wankuru aliongeza kwa kusema “kujishindia unatakiwa kujinga na kifurushi chochote cha Airtel yatosha cha siku, wiki au mwenzi kwa kupiga 14999# au kununua vocha  ya Airtel yatosha au kwa kununua kupiita huduma ya Airtel Money, baada ya kununua kifurushi chako namba yako moja kwa moja itaingizwa kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”.

Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi ilizinduliwa na kampuni simu za mkononi ya Airtel Mwanzoni mwa mwenzi wa Februari, watanzania wengi kutoka katika mikoa mbalimbali wameweza kujishindia magari na kubadili maisha ya kupitia promosheni hii. Magari 24 yameshapata washindi toka promosheni hii ianze hadi sasa.

Tupia Comments