Michezo

Wakati Mata akiwasili Old Trafford, Zaha afanyiwa vipimo kujiunga kwa mkopo na Cardiff City

on

Wilfried-Zaha-Manchester-United_2984853Winga wa Manchester United Wilfried Zaha anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Cardiff City kwa muda wote wa msimu uliobakia, gazeti la Manchester Evening News limeripoti.

Zaha, ambaye alijiunga na United akitokea  Crystal Palace kwa uhamisho wa 15 million-pound mwaka jana, amefanyiwa vipimo vya afya na timu hiyo inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa United Ole Gunnar Solskjaer.

Gazeti hilo linaripoti kwamba mchezaji huyo ameonekana akiingia kwenye hospitali huko Cardiff kwa ajili ya kufanyiwa vipimo. Ikiwa uhamisho huo utafanikiwa, anategemewa kwamba ataweza kuanza katika mchezo wake wa kwanza na Cardiff dhidi ya Norwich City mnamo Feb. 1. United na Cardiff zinakutana wiki ijayo lakini Zaha hatokuwa akiruhusiwa kucheza kwenye mchezo huo.

Tupia Comments