Duniani

PICHA 17: Tazama Mabasi ya Brazil, vituo vyao na usafirishaji wa abiria wa ‘mikoani’

on

Brazil ni moja ya nchi maarufu duniani na ni taifa lililotajwa kushika nafasi ya tano kwa wingi wa watu duniani ambapo mpaka mwaka 2015, idadi ya watu ilikua ni zaidi ya milioni mia mbili huku rekodi za mwaka 2010 zikionyesha kwamba taifa hili lilikua na asilimia 7 ya raia Weusi.

Moja ya vitu nilivyovipenda Brazil ni walivyojipanga kwenye usafirishaji…. wingi wa watu haujafanya vituo vyao vya Mabasi viwe vichafu au visivutie, sheria za Mabasi yanayotumika ndio kama yanayoonekana kwenye picha na barabara zao za umbali mrefu zimetenganishwa kwa umbali kiasi kwamba hakuna uwezekano wa magari kugongana uso kwa uso.

Kwenye haya mabasi mfano ukisafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine hakuna kondakta ndani, Dereva ndio anafanya kazi ya kuhakiki majina ya kila anaeingia kwenye basi baada ya kununua Ticket baada ya hapo ni safari tena Mabasi mengi yakiwa na huduma ya WiFi ndani, yani Internet unaipata bure safarini na mabasi yote ni sharti yawe na choo ndani.

b17

Vituo vya Mabasi vimezibwa kwa juu hivyo hata mvua ikinyesha sio tatizo Abiria kushuka au kupanda kwenye basi.

b16

Mabasi haya ni ya gorofa, ukiwa na uwezo zaidi unalipia kukaa kwenye sehemu yenye hadhi zaidi ndani ya basi ambako mnakaa wachache na unanafasi ya kulala na kujisevia vinywaji.

b15

b14

Abiria wanakaa juu na chini na niliambiwa kwa chini ndio unalipia pesa nyingi zaidi na mnakaa wachache.

b13

b11

b9

b12

b8

Hapa ni ndani ya kituo cha Mabasi kwenye mji wa Sao Paulo

b7

b6

b5

b4

Sehemu za kukata ticket ndani ya kituo

b3

b2

B1

ULIIKOSA VIDEO NA STORI YA DALADALA KUANZA KUPITA DARAJA LA KIGAMBONI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments