Habari za Mastaa

R.Kelly ajisalimisha mikononi mwa polisi mjini Chicago (+video)

on

Mwanamuziki R. Kelly (52) amejisalimisha katika kituo cha polisi mjini Chicago usiku wa February 22,2019, R.Kelly anashtakiwa kwa kosa la kuwanyanyasa kingono wanawake 10 ambao watatu kati yao walikuwa chini ya umri wa miaka 17 .

Inaelezwa kuwa R.Kelly aliondoka studio kwake na kuelekea polisi na mpaka sasa taarifa zinaripotiwa kuwa tayari R.Kelly yupo rumande baada ya kufikishwa mikononi mwa polisi mjini Chicago na hivyo atafikishwa Mahakamani March 8,2019.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Kim Foxx amethibitisha kuwa makosa 9 kati ya hayo 10 yanahusu unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wenye umri wa miaka 13 hadi 16 na ni kuanzia mwaka 1998 mpaka 2010.

‘NILIKUNYWA DAMU YA KUKU NA KUUZA MALI ZANGU ZOTE’ – HAFSA KAZINJA

Soma na hizi

Tupia Comments