Top Stories

Hukumu waliyopewa waliochoma BIBLIA na kukata watu Koromea Kagera

on

Leo June 8, 2018 Mahakama ya wilaya Bukoba imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka mitano pamoja na kulipa faini huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa makosa ya awali ya kuchoma makanisa na kuharibu mali za kanisa na hukumu hiyo ilitolewa December 2017 .

Waliohukumiwa ni Rashid Mzee miaka 33, Ngesera Care 31 na Alliu Dauda 34, ambapo walikuwa wanakabiliwa na makosa ya kula njama ya kutenda kosa, kosa la uharibifu wa vitu ambavyo ni mali ya kanisa la Pentecostal.

Akizungumza na AyoTV na millardayo.com Wakili wa serikali mkoa wa Kagera, Haruna Shomary amesema kuwa vijana hao tayari wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya awali ambayo yanawakabili na wanakabiliwa na mashtaka manne ikiwa ni pamoja na kesi ya mauaji kwa kutoa watu Koromeo.

Tazama LIVE mapya aliyoibuka nayo Dr. Shika akizungumza na Waandishi ‘Tutaelewana’

 

Soma na hizi

Tupia Comments