Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Siku 3 baada ya kuanza Kombe la Dunia Urusi, dereva agonga watembea kwa miguu

on

Leo June 18, 2018 Dereva mmoja wa teksi nchini Urusi ametiwa mbaroni hapo jana baada ya kupatikana akiliendesha gari lake kwenye njia ya waenda kwa miguu na kuwajeruhi watu saba mjini Moscow.

Mwanaume huyo wa mwenye miaka 28 kutoka eneo la Kyrgyzstan, alipoteza udhibiti wa gari hilo kabla ya kuwagonga watu hao na kukimbia kutoka kwa eneo la tukio hilo kabla ya kukamatwa na maafisa wa polisi muda mchache baadaye.

Ripoti zaidi zinasema, kijana huyo alikuwa amelala tukio hilo lilipotokea na kuwa alikuwa amefanya kazi kwa zaidi ya masaa 20 bila kupumzika.

Ajali hiyo ilitokea siku ya tatu ya michuano ya kombe la dunia mjini Moscow.

Usalama umeimarishwa nchini Urusi kufuatia michuano ya kombe la dunia inayoendelea ambapo jumla ya watalii 600,000 wanatarajiwa kuitembelea nchi hiyo.

LIVE MAGAZETI: Zitto: Bajeti inatia shaka, Basi la Mbunge Msukuma lauwa watano

Soma na hizi

Tupia Comments