Habari za Mastaa

Shabiki amtishia Rude Boy wa P Square kumuua kisa pesa za kwenda Marekani

on

Msanii kutokea Nigeria Paul Okoye a.k.a Rudeboy wa P Square ameweka wazi kile ambacho aliandikiwa na shabiki yake kutokea Kenya kama ambavyo imezooleka kwa wasanii kupokea jumbe tofauti tofauti kutoka kwa mashabiki zao kupitia mitandao ya kijamii.

Shabiki huyo ambaye alijatambulisha kwa jina la Morah’ 22 na kusema kuwa yeye ni Mkenya lakini kwa sasa makazi yake yapo Tanzania angeomba Paul amsaidie kifedha ili aweze kwenda kumalizia masomo yake Marekani na angependa amlipie safari ya kwenda tena Marekani mwezi huu wa June kwa ajili ya mapumziko.

Baada ya kuona kuwa Paul hajatekeleza maombi yake aliamua kumtumia tena ujumbe na kumuambia kuwa amechelewa kufanya kile ambacho alimuomba na kusema kuwa atamuua kama ambavyo angewaua watu wenye roho mbaya kama yeye aliendelea kusema kuwa Mungu angependa kuona Paul anakufa na watu wengine waovu.

“Paul Okoye umechelewa toka haujanipa kile ambacho niliomba wewe ni muovu, Mimi Morah nitakuua kama ambavyo nitauua watu wengine waovu , Mungu anataka wewe pamoja na watu wengine waovu kufa , hautojua siku zako za kufa tunza uovu, uchafu, tunza hela zako, Nenda peponi Paul “ >>>aliandika shabiki huyo

Paul Okoye aliamua kuandika “Binadamu wengine ona, moto wako utakua V.V.I.P labda nafasi ya pili itakuweka pale”

VIDEO: ULIIPATA HII YA KALA JEREMIAH KUZUNGUMZA, ASLAY KAMRINGIA KUTOTOKEA KWENYE VIDEO YAKE..? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments