Stori ya mashabiki kujiua eti kisa timu yake imefungwa ama ina matokeo mabaya kwenye ligi sio ngeni kuzisikia.. Wapo ambao wanashindana wanaweka nyumba au hela, timu yake ikishindwa ishu inakuwa story tofauti.
Taarifa kutoka Kaunti ya Kilifi pwani ya Kenya mtu moja amejitoa uhai kwa kujitosa ndani ya bahari hindi kutoka kwa Daraja la Kilifi baada ya kukasirishwa na matokeo ya Robo fainali kombe la FA baina ya mahasimu wakubwa Uingereza Arsenal na Man United iliyochezwa jumanne usiku.
Mtu ambaye alizungumza na jamaa ambaye amejiua amesema kabla ya mechi shabiki huyo alikuwa akijigamba jinsi Man U watakavyowaadhibu Arsenal, lakini hali ikawa tofauti.
Ishu iko mikononi mwaPolisi ambao wanendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook