Kwenye zilizopewa Headlines Magazetini leo March 17, iko ya TAKUKURU kuanzisha mfumo na utaratibu wa kuwatangaza hadharani washtakiwa waliokutwa na hatia ya kesi zinazohusu rushwa, Mchungaji Christopher Mtikila kufungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Damian Lubuva amesema Kenya na Nigeria zimegoma kuiazima Tanzania mashine za BVR.
Kwenye uchambuzi wa Magazeti kulikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa TAKUKURU Dr. Edward Hosea ambae amesema watu watakaokutwa na hatia kwa kuhusika na rushwa watatangazwa hadharani, ikiwa ni mkakati mpya ulionzishwa na Serikali kuonyesha ni jinsi gani inachukua hatua dhidi ya mapambano ya rushwa, ambapo majina hayo yatawekwa katika mtandao wa PCCB.
88.0 Clouds FM inasikika ukiwa Tabora.
Bonyeza play kusikiliza Uchambuzi wa Magazeti ya Leo
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook