Jumamosi iliyopita kuliripotiwa kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi katika milima ya Everest, Nepal ambapo si mbali na makazi ya watu.
Katika tukio hilo magazeti yaliyotoka leo yana taarifa kwamba watu 2000 wamefariki pamoja na majeruhi zaidi ya watu 5000.
Mwndelezo wa habari hiyo unasema mpaka sasa idadi ya watu waliofariki ni 3,600 na huenda idadi ikaongezeka wakati wowote kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya.
Idadi kubwa ya watu ambao wanaishi karibu na milima wako katika hali mbaya na kukosa makazi.
Athari zilizojitokeza bado ni kubwa sana.. wapo watu wengi waliokosa makazi, wengine waliamua kulala kwa zaidi ya siku mbili nje kabisa ya nyumba zao huku wengine wakilala kwenye mahema yaliojengwa kwa mifuko ya plastiki.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook