Shughuli ya kwanza iliyompeleka Dodoma Rais Kikwete Dodoma ameikalimilisha leo July 09 2015, ilikuwa alihutubie Bunge pamoja na kulivunja Bunge hilo ambapo Wabunge wanarudi Majimboni kwa ajili yakuendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa October 2015.
Hotuba yake imechukua zaidi ya saa mbili, najua kuna waliopitwa na hii, niliiredoki yote na unaweza kuisikiliza hapa pamoja na kusoma baadhi ya nukuu za maneno yake kwenye kile alichokisema.
‘Mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi ya ujambazi, niliahidi kwamba hatutawaacha.. Hali imedhibitiwa’- #RaisJK#BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Natoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa wanayofanya’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Jambo ambalo hatujafanikiwa ni tatizo la ajali za barabarani, nalo tunalitafutia mwarobaini’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Mazingira ya Magereza TZ yameboreshwa, tatizo kubwa kwa sasa ni msongamano wa Wafungwa ktk Magereza’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nawapongeza Wabunge walioshiriki ktk Mafunzo ya JKT.. Wameonesha mfano mzuri’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Bunge limefanya kazi kubwa, mnastahili pongezi, huwezi kutaja mafanikio ya Serikali bila kutaja mchango wa Bunge’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Napongeza Tume ya Katiba na Bunge kwa kufanikiwa kuipata Katiba iliyopendekezwa, ninaamini tutapata Katiba nzuri’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Vyama vya Siasa vimeongezeka na kuimarika, vimekuwa huru kufanya mambo yao hata kutoka Bungeni’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Habari kubwa kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu, watu zaidi ya Mil. 11 wameandikishwa kati ya watu Mil.23’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Naamini kila mwenye sifa ya kuandikishwa na kupigakura atapata nafasi hiyo, labda aamue kukataa mwenyewe’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘TZ kuna jumla ya Magazeti 16, ya Serikali ni mawili.. Hakuna Uhuru wa Habari?’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kuna Radio 115, radio ya Serikali ni moja.. TV zaidi ya 20, TV ya Serikali ni moja.. Hakuna uhuru wa Habari?’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Sheria ya Vyombo vya Habari ilitungwa lakini haikufanikiwa kupitishwa, tunaachia Bunge lijalo lije kumalizia kazi’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tulitoa kipaumbele kwenye Mapato na Matumizi.. Mapato yameongezeka, tunakusanya zaidi ya Bil.800 kwa mwezi’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Naamini mpaka mwisho wa mwaka huu tunaweza kufikia kukusanya mpaka Trilioni 1 kwa mwezi’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeimarisha Ofisi ya CAG kwenye kufanya ukaguzi, Kamati ya Bunge nayo inafanya kazi nzuri na wezi wanawajibishwa’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Niliagiza kama kuna mbadhirifu kwenye Ripoti ya CAG, aripotiwe Polisi na TAKUKURU wakati Ripoti inaenda Bungeni’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Hati chafu zinapungua, hati safi zimeongezeka, huwezi kutoa pesa alafu usiulize matumizi, inakuwa kama unapeleka ubani msibani’- #RaisJK — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nilikutana na Majaji wakaniambia mipango yao kila Jaji anatakiwa kusikiliza mashauri zaidi ya 220 kwa mwaka’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nimeamua kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe kwa kuugawa Mkoa wa Mbeya’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Katika kipindi chote karibu kila mwaka tumeongeza kima cha chini cha Mshahara, najua hakitoshi ila tunasogea’– #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Niliahidi kuongeza ushiriki wa Wanawake ktk shughuli mbalimbali ikiwemo maamuzi,hata Wabunge wanawake wameongezeka’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kwa mara ya kwanza tumempata Spika wa Bunge mwanamke, wako Mawaziri, Makatibu Wakuu na kwingineko’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kwenye shule za Msingi, Sekondari na Vyuoni nako kuna ongezeko kubwa la wanafunzi wa kike’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘TZ ni ya saba Afrika na ya 20 duniani ktk Nchi zinazokua kwa kasi.. Pato la Taifa nalo limeongezeka’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘IMF wanasema pato la Mtanzania ni kubwa kuliko inavyosemwa, tumebakiza kidogo kufikia pato la kati’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘TZ inaongoza ktk nchi za Afrika Mashariki kwa kuvutia Uwekezaji kwa mujibu wa Ripoti ya 2015’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumezindua mpango AU kwamba jembe la mkono lisiwe zana ya kilimo, lirudishwe kwenye Makumbusho’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeongeza uzalishaji wa Chakula na TZ inaweza kujitosheleza chakula kwa 120%’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeendeleza sekta ya Utalii, inachangia 25% ya Mapato ya Fedha za Kigeni.. ndio sekta inayoongoza TZ’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Ujangili ulifikia hatua ya kutishia kumaliza tembo sio TZ pekeake, ila duniani kote’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Zilifanywa Oparesheni tatu tofauti kukabiliana na Ujangili, hivi sasa hali inaridhisha hifadhi za TZ’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Sekta ya Viwanda nayo inafanya vizuri, mwezi ujao tunaweka jiwe la Msingi kiwanda cha Chuma’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Viwanda vya Chuma na Gesi vikianza kazi vitasaidia kuinua Uchumi, hata tukisema Tanzania paa inapaa’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kupunguzwa kwa misamaha ya Kodi kumesaidia sana kuongezeka kwa Mapato TZ kutoka sekta ya Madini’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Vijiji zaidi ya 5,300 vimepatiwa umeme kutokana na mradi wa REA, Watz wanaopata umeme kwa sasa ni 40%”- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘TZ ni moja ya nchi zenye Gesi nyingi Duniani, Mapato yake yakisimamiwa vizuri yatasaidia kuinua Uchumi”- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nashukuru Wabunge kwa kupitisha Miswada ya Gesi na Petroli, mkiniletea naisaini wakati huohuo’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeboresha barabara za TZ, ukitokea sehemu yoyote TZ unafika DAR ndani ya siku moja, tofauti na ilivyokuwa nyuma”- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Bajaji, magari na pikipiki vimeongezeka pia, ongezeko hili linatokata na hali nzuri ya Kiuchumi kwa watu’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Ongezeko hilo limechangia pia kuongeza misongamano barabarani, Serikali inafanya mipango kumaliza tatizo hilo pia’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumepanua barabara,tumetumia treni kwenye maeneo kama Dar,zitajengwa na barabara za juu maeneo ya TAZARA na Ubungo’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Mizigo ikiendelea kusafirishwa kwa magari, barabara hazitadumu muda mrefu, tuna mpango kufufua usafiri wa Reli’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumefanya mazungumzo na Zambia na Wachina ili kuifufua Reli ya TAZARA’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeiboresha Bandari ya DAR, sasa hivi inafanya kazi kwa saa 24.. wizi nao umepungua’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumekarabati Viwanja vya Ndege, JNIA inapokea mpk ndege 30 kwa sasa’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Abiria wanaotumia Ndege wameongezeka, hata Watz nao wanapanda Ndege kwa sababu hali ni nzuri’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Hatujaweza kulifufua Shirika la Ndege, tuko kwenye mpango kuamua jinsi ambavyo tunaweza kulifufua Shirika hilo’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa na sasa taarifa zake zinatambulika popote duniani’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Watumiaji wa simu wameongezeka kutoka Mil.2 mwaka 2005, mpaka Mil. 28.. Watumiaji wa Internet kwa sasa ni Mil.12’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘TZ ni nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuhama kutoka mfumo wa Analogy kuwa Digital,wenzetu wanakuja kujifunza kwetu’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Takwimu za 2012 zimeonesha nyumba za mabati zimeongezeka za makuti na nyasi zimepungua.Ukipita juu kwa ndege unaona’- #RaisJK BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Hakuna Taifa limeendelea bila Elimu, tumetimiza ahadi kwa kuboresha Elimu.Mafanikio yaliyopatikana yanatia moyo’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kuna ongezeko kubwa la vyuo Vikuu na vinaendelea kujengwa. Wanafunzi wanapata Mikopo pia wameongezeka’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Huduma za Kiafya nazo zimeboreshwa, Hospitali na Maabara zimeboreshwa ikiwemo Hospitali za Rufaa na Mikoa’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Hospitali ya Mbeya ina maabara ya kupima EBOLA, kipindi cha nyuma ilikuwa ni lazima vipimo vikafanywe Nairobi’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumegawa vyandarua vingi ili kupambana na Malaria, vimekuwa vingi wengine wanafugia na kuku’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kuna ongezeko la Madaktari, kwa sasa wako zaidi ya 2,000.. Umri wa kuishi TZ umeongezeka mpaka miaka 62;’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Niliahidi kukuza Michezo na sanaa, kwenye Michezo Serikali imelipia Makocha kwenye kila mchezo’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kwenye kulipia Makocha mpira wa miguu ndio zaidi, kila wakifukuza akija mwingine tunamlipa’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Timu ya Taifa haifanyi vizuri, walisema kila nikienda wanafungwa.. nikaacha kwenda Uwanjani lakini bado wanafungwa’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Mwaka 2014 niligharimia Timu ya wazoefu kutoka Marekani kuja kutoa mafunzo kwa wasanii wa Muziki na Filamu’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Ninafanya mpango warudi tena.. Wanamuziki niliwapatia Studio, kwa sasa tuna mkakati kuendelea kusaidia wasanii’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tukipata maumivu kwenye soka, muziki na movie vinatuliwaza..Wasanii wa muziki na movie wanafanya kazi nzuri kuitangaza TZ’- #RaisJK — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tumeweka rekodi kutembelewa na Marais wawili wa Marekani, wengine wanatamani hata mmoja haendi’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kila Kiongozi Mkubwa Duniani ametembelea Tanzania’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tulipanga kufanya mengi lakini hatukuweza kuyafanya yote.. Tumefanikisha kutekeleza 88% ya ahadi za Serikali’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Tulipo sasahivi ni bora zaidi kuliko tulipokuwa jana.. Hata Hayati NYERERE, Mzee MWINYI na MKAPA hawakumaliza yote’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Kinachonipa faraja ni kwamba na mimi nimefanya kitu kwenye kuchangia kukua kwa nchi yetu’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Napenda kumshukuru Mizengo PINDA kwa mchango wake, wakati mwingine alibeba lawama zisizo zake’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Namshukuru pia Edward LOWASSA alifanya kazi nzuri wakati wa Uongozi wake kama Waziri Mkuu’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nawashukuru Viongozi wote, Mawaziri, na mwisho kwa familia yangu’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nawashukuru wanangu na wajukuu zangu, kuna wakati waliniuliza kwanini sina muda wa kuwa nao?’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Nawashukuru walioonesha nia kunipokea mzigo mzito wa Urais, ila mko wengi tena Vigogo watupu’- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Leo tunafanya kama Sendoff, harusi yenyewe ni tarehe 20 September’- #RaisJK #BungeniDODOMA
— millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
‘Ninawapenda sana na nitawapenda mpaka siku Mwenyezi MUNGU akiniita.Navunja Bunge ila litakuwa hai mpaka September”- #RaisJK #BungeniDODOMA — millard ayo (@millardayo) July 9, 2015
Sauti ya hotuba yote ya Rais JK iko kwenye hii sauti hapa, bonyeza play kama ulipitwa umsikilize.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.