Ulisikia kwenye majukwaa ya kisiasa Wapinzani wakisema kwamba shirika la ndege Tanzania limekufa? sasa Waziri wa uchukuzi Samwel Sitta baada ya kuyasikia hayo amesimama kuyatoa haya mbele ya Waandishi wa habari.
Waziri Sitta anasema shirika la ndege halijafa kama wapinzani wanavyodai na kwamba serikali ipo kwenye mkakati wa kulipa deni ili iweze kukopesheka na baadae shirika lijiendeshe kwani ndege moja haitoshi.
Anasema >>> ‘Wahandisi na Marubani wapo na wanaendelea kulipwa kama kawaida mpaka ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2015 shirika litakua limepata ndege na kuanza safari zake kama kawaida pamoja na usafiri wa reli ya kati serikali ina mpango wa kuikarabati kuifanya reli ya kisasa‘
‘Kuhusu wafanyakazi wa Air Tanzania kuendelea na kazi pamoja na kwamba hakuna ndege, kwenye taaluma flani kuna vigezo vimewekwa ambavyo lazima vifuatwe amasivyo Muhusika anapoteza sifa mfano Rubani, anatakiwa kila mwezi arushe ndege kwa saa flani kwahiyo ukitaka kubakia na Pilot ni lazima uwatengenezee mazingira ya hata ndege nyingine wabaki kama waajiriwa wako ili ikipatikana ndege waweze kurusha manake Pilot asiporusha ndege kwa muda flani unashushwa kiwango mpaka uende mafunzo tena‘ – Samwel Sitta
‘Sisi tuna shirika tayari lina ndege hiyo moja ni lazima tubaki na Wahandisi na Marubani ili tukiwa tayari shirika liendelee tu na kazi bila kulazimika kuanza upya kabisa, hasara kubwa zaidi ni ingekua ni kwamba uko tayari na ndege za bei kubwa kabisa umeziagiza zipo hapa na Marubani wako wote hawana sifa za kuziendesha’ – Samwel Sitta
MSIKILIZE SAMWEL SITTA KWA KUBONYEZA PLAY HAPA
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos