Kuna kitu kingine nimekifahamu leo baada ya Peter Okoye, mmoja ya mapacha wanaounda Crew ya P Square kuandika kuhusu ishu ni Kituo cha TV cha Soundcity kuacha kupiga nyimbo zao !!
Kuna ukweli kwenye hilo, yani TV ya Nigeria iache kupiga Video za mastaa wa nyumbani kwao kabisa ?
Hizi ni #TWEETS nne za Peter wa P Square kuhusu ishu ya TV ya Soundcity kutocheza Video zao.
Kwenye majibu yaliyotolewa na Kituo cha TV cha Soundcity, wametoa sababu ya kutopiga video za P Square.
Ishu ilianzia December 2014 ambapo TV ya Soundcity iliwaalika P Square kwenye event yao, kwenye makubaliano ya kiasi cha pesa ambacho P Square walihitaji kulipwa, Sound City walihitaji majadiliano ili wapate punguzo la bei !! Jibu la Manager wa P Square ambae ni kaka yao mkubwa, Jude ‘Engees’ Okoye hawakulipenda.
‘Nini mmewahi kukifanya kwa P Square? naomba mniambie hata kitu kimoja mlichowahi kuwafanyia P Square?’- Hii ni nukuu ya alichokojibu Manager wao, Jude Okoye.
Hili jibu halikuwafurahisha, kwa sababu Soundcity wamesema wamekuwa na support kubwa sana kwenye Muziki wa P Square toka wakiwa wanaanza muziki, na kuna wakati watu walilalamika kwamba Video za P Square zinapigwa sana mpaka inakera watu wanaoangalia Soundcity TV !!
Soundcity wamesema kwamba sio hilo tu, kuna wakati P Square walifanya tour ya muziki Africa kwa gharama za TV hiyo… matangazo na kila kitu hawakulipia gharama yoyote, hili la leo kuambiwa hawajafanya chochote haikuwa kitu ambacho walifurahia hata kidogo…
Waliacha kurusha Video za P Square January 2015 na hawana ubaya nao, wanawatakia heri kwenye muziki wao na wako tayari kutoa support ya nguvu kwa kila msanii mchanga ndani ya Africa ili muziki wa kila msanii uendelee kukua.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos