Alhamisi ya tarehe 17 September 2015 imeanza na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM, na kwenye stori zilizoweka headlines zipo hizi ambazo zimesikika kwenye #PowerBreakfast…
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli asema “M4C” inamaanisha “Magufuli 4 Change” akimaanisha ndiye atakayeleta mabadiliko, Edward Lowassa ameahidi kufufua viwanda kwenye wilaya ya Chato mkoani Kigoma kama akipewa ridhaa ya kuongoza nchi.
CCM imesema utafiti wake wa ndani uliofanyika kwenye majimbo 256 unaonyesha mgombea wao wa Urais Dk. John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu kwa 69.3%, TLP imeiomba NEC tarehe ya Uchaguzi Mkuu kuwa tarehe 26 badala ya tarehe 25 October ili kuwasaidia wakristo kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Kamishna mpya wa NEC Judge Mary Longwe ameahidi kutenda haki kwa kila mgombea kwenye Uchaguzi Mkuu October 25, Zitto Kabwe amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mafanikio yaliyopatikana Mkoa wa Kigoma wakati wa uongozi wake.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi asema ataongoza mahujaji wa Tanzania kuombea uchaguzi mkuu uwe wa amani atakapofika kwenye mji mtakatifu wa Mecca, majaribio ya mfumo mpya tozo za papo kwa papo kwa njia ya kielektroniki kuanza kutumika leo kwenye baadhi ya maeneo ya Dar es salaam.
Hapa chini nimeiweka sauti yote ya uchambuzi wa magazeti bonyeza play kusikiliza.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos